Mwongozo wa Mapambazuko ya Machweo na hadithi nyingine

KSh 90

uchambuzi wa hadithi zote za Mapambazuko ya Machweo. Mtiririko, Ufaafu wa Anwani, Dhamira ya Mwandishi, Maudhui, Wahusika: Sifa na Umuhimu, Mbinu za Uandishi. 209 pages.

Download

Description

1. Toba ya kalia

• Mtiririko
• Ufaafu wa Anwani ‘Toba ya Kalia’.
• Dhamira ya Mwandishi
• Maudhui
• Wahusika: Sifa na Umuhimu.
• Mbinu za Uandishi

Mtiririko
Jack anapokea simu ya Kalia, babake Siri, rafikiye mkubwa tangu utotoni.
Ujumbe ni kuwa Siri atakuwa hewani kwenye runinga ya Kikwetu, na ameagiza Jack na wazazi wake (Siri) wawepo. Anavaa shati alilolainisha kwa kuweka chini ya godoro na suruali ya khaki.Hali hii ni kwa kuwa anawekeza kujiendeleza kimasomo.
Safarini, Jack anakumbuka baruapepe ya Siri akimweleza angetumia fursa hiyo kupitisha ujumbe aliotaka ulimwengu usikie. Siri huwasiliana na wazazi wake kupitia skype, na Jack ndiye huwasaidia kuunganisha mitambo, licha ya kuwa amekomea shule ya upili kimasomo. Wanaketi ukumbini wa mahojiano na kukaribishwa kwa sharubati.
Kiswahili cha binti mtangazaji kinamfurahisha Bi. Mshewa, mkewe Kalia kwani ni mwalimu wa Kiswahili.
Jane Gatoni, mtangazaji, anawakaribisha watazamaji katika kipindi chao, Nyumbani ni Nyumbani na kuwatambulisha wageni……………

error: Content is protected !!